Wednesday, December 12, 2012

KICHEKESHO-HUYU KAMA KUJISIFIA ANASTAHILI TUZO...msome hapa!!..

Jana jumapili jioni alisikika
MHAYA mmoja pale
Jamaa akiongea kwa sauti mbele
za watu.
"Aise dreva wangu, hebu nenda
kwenye nyumba
yangu ile nyekundu, siyo ile ya
Bunju, wala sio ile ya
Kunduchi, ila ile ya Masaki....
Lakini usiende ile ya
Chole Road, wala ile ya Msasani
Road, nenda ile ya
Kenyatta Drive!!!
Fungua geti lile jeusi la chuma ,
tumia rimoti
usifungue vingine.... Ukiingia
utakuta VX yangu,
achana na hiyo angalia ile Benz ya
Bluu ambayo
pembeni yake kuna BMW... Sasa
pembeni kidogo
utaona HUMMER NYEUSI, fungua
buti, utakuta mabegi
ya hela kuna moja lina EURO acha
hilo, wala
usichukue yale yenye POUND.....
Fungua moja kati ya yale yenye
noti za dola mia mia,
utakuta funguo za mabriefcase
yangu ambayo yako
ndani.... Ukishachukua funguo
nenda mpaka ghorofa
la 3, ingia chumba anacholala
mbwa wangu yule
KOKU ambacho ni kile chumba
cha pili, acha kile
ambacho zamani walikuwa
wanalala PAKA...
Ila plzzzz, ukifika gonga mara tatu
kama mbwa
wangu koku atakuwa hajalala
ingia chumba cha pili
ambacho wanacholala watoto
wake... Angalia vizuri
coz kinafanana na cha mama yao
ambacho ukiingia
chini ya ile plazima TV utakuta
meza ina decoda na
playstation 3, sasa kwa pembeni
utaona briefcase 3,
moja lina noti za elfu 5 5, la pili
lina noti za elfu 10 10
na la tatu lina elfu 2 2... Chukua
sasa noti za elfu
kumi kumi kana laki tano....
Ila hakikisha wale watoto wa
mbwa wanabugger za
kutosha kitandani kwao kabla
hujatoka.... Then
ukishachukua naomba
ukaninunulie chupa 3 za maji
pale kiwandani COCA COLA
KWANZA uniletee...
Sawa!?!?"
GetMore.com By George Mophaty

No comments:

Post a Comment